VIDEO:: KAMA BADO HUJAONA MABAO YA YANGA VS NJOMBE MJI, HAYA HAPA


Ligi kuu Tanzania bara iliendelea leo Jumanne Februari 6, 2018, kwenye uwanja wa uhuru jijini dar es salaam umechezwa mchezo kati ya yanga dhidi ya njombe mji na kushuhudia mchezo huo ukimalizika huku yanga wakipata ushindi wa magoli 4-0 na kuendelea kuinua matumaini ya kutetea taji lao la ligi.
Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa ameng’ara katika mchezo huo baada ya kufunga magoli matatu ‘hat-trick’ huku goli jingine likifungwa na Emanuel Martin. Yanga imefikisha pointi 34 ikiendeleza vita ya kuwania taji VPL dhidi ya Singida United, Azam na Simba ambao wanashikilia nafasi ya kwanza kwenye msimamo.

BOFYA HAPA KUTAZAMA VIDEO




No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.