RATIBA YA LEO JUMAMOSI, LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA



LIGI kuu Tanzania Bara raundi ya 15 inayokamilisha mzunguko wa kwanza inatarajiwa kuendelea leo Jumamosi kwa michezo minne kupigwa katika viwanja tofauti.

Baada ya mchezo wa juzi na jana ligi kuu itaendelea leo ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo Young Africans watakuwa wageni wa klabu ya Azam Fc majira ya saa 16:00 jioni katika uwanja wa Azam complex (Chamanzi).Kuelekea kwenye mchezo huo klabu ya Yanga utawakosa nyota wake saba, ambapo ni Pius Buswita anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njao, Pato Ngonyani Thaban Kamusoko, Amissi Tambwe, Yohana Nkomola, Abdallah Shaibu "Ninja" na Donald Ngoma.

Afisa Habari wa Yanga amesema kuwa wachezaji hao ni wagonjwa kasoro Buswita ambaye ana kadi tatu za njano.


Azam wao wamesema kuwa wachezaji wao wako vizuri na wako katika maandalizi mazuri na kiafya, kiakili wako vizuri na wanataka kuwahakikishia mashabiki wao kuwa wanatimiza ile adhma yao katika kulinda heshima ya uwanja wetu wa Azam Complex kwamba hatuhitaji kufungwa hapa na leo vijana wako sawa na watafanya lile tulilolipanga nao," alisema Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche.

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 16:00 jioni katika uwanja wa nyumbani wa Azam Complex (Chamanzi), huku viingilio vya mchezo huo vikitajwa kuwa ni elfu 10,000 VIP na elf 7,000 kwa mzunguko.

Mechi nyingine za leo Jumamosi zitakuwa kati ya wanankurukumbi Kagera Sugar watakaowakaribisha Lipuli Fc ya Iringa saa 16:00 jioni katika uwanja wa Kaitaba-Bukoba.

Mtibwa Sugar watakuwa wageni wa Mbeya City saa 16:00 jioni katika uwanja wa Sokoine-Mbeya.

Mwadui Fc watakaowakaribisha Njombe Mji ya Njombe saa 16:0) jioni katika uwanja wa Mwadui Complex-Shinyanga.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.