NI RONALDO TENA, TUZO YA FIFA KWA MARA NYINGINE TENA.
Kwa mara ya pili Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya The Best Fifa awards baada ya kupata 43% ya kura zilizopigwa huku akimuacha mbali mpinzani wake mkubwa Lioneil Messi aliyepata 19%.
Msimu uliopita Cristiano Ronaldo alifunga mabao 12 katika Champions League huku akifunga mara mbili katika mchezo wa fainali na kuwasaidia Real Madrid kutetea kombe la Champions League.
Manahodha waliompigia kura Cristiano Ronaldo ni pamoja na Luca Modric, Sergio Ramos, na Marcelo huku Neymar, Iniesta na Suarez wakimpigia kura Lioneil Messi.
Wakati Ronaldo akitwaa Best Male awards kocha wake Zinedine Zidane aliwabwaga Massimiliano Allegri na Antonio Conte na kutwaa tuzo ya kocha bora wa FIFA.
Gianluigi Buffon alichukua tuzo ya golikipa bora akiwabwaga wapinzani wake golikipa wa Real Madrid Keylor Navas na golikipa wa Bayern Munich Manuel Neuer.
Olivier Giroud alipata tuzo ya bao bora huku kikosi bora cha Fifa kikiundwa na Gianluigi Bufgon, Dani Alves,Leornardo Bonuccci, Sergio Ramos, Marcelo,Toni Kroos, Andres Iniesta, Luvca Modric, Cristiano Ronaldo, Lioneil Messi na Neymar.
Tuzo zingine zilizotolewa usiku wa leo ni tuzo ya mchezaji bora wa kike iliyokwenda kwa Lieke Mertenes, tuzo ya kocha bora wa kike ikienda kwa Sarina Wiegman na tuzo ya mashabiki ikienda kwa mashabiki wa Celtic.
No comments