MJUE KIUNDANI ZAIDI MRITHI WA JACKSON MAYANJA NDANI YA MSIMBAZI




Baada ya aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja kujiuzulu nafasi hiyo, kocha Masud Djuma raia wa Burundi anatajwa kuziba nafasi hiyo.
Djuma amepata mafanikio akiwa kama kocha na kuishawishi Simba kumsaini kuwa msaidizi wa Joseph Omog kwenye benchi la ufundi la Simba.
Msimu uliopita Djuma alikuwa kocha wa Rayon Sports ya Rwanda na kuisaidia timu hiyo kutwa aubingwa ligi kuu. Badae akachaguliwa kuwa kocha bora wa msimu 2016/2017.
Amewahi kuvichezra vilabu vya APR, Rayon Sport, Prince Louis, Inter Star pamoja na timu ya Taifa ya Burundi ‘Intambamurugamba’.
Alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Burundi kilichoshiriki mashindano ya FIFA ya vijana (FIFA World Yourth Championship) mwaka 1995 nchini Qatar. Alicheza mechi tatu katika mashindano hayo.
Inaelezwa Djuma ni kipenzi cha wachezaji kutokana na ukatibu wake na kuwafanya wachezaji marafiki zake, huwa anavaa jezi na kujumuika pamoja kwenye mazoezi na wachezaji.
Amezaliwa August 30, 1977 Bujumbura Burundi, kwa sasa ana miaka 40. Bado kijana mwenye nguvu za kuweza kukimbizana na wachezaji mazoezini.
Inategemewa akatambulishwa rasmi leo October 19, 2017 mbele ya waandishi wa habari kwenye mkutano maalum wa Simba na vyombo vya habari makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi, Dar.


No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.