MAKALA: TOFAUTI 7 ZA IBRAHIM AJIB NA OKWI, TUKUTANE KESHO TAIFA
Wakati joto likizidi kupanda kuelekea Dar derby baina ya mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga SC dhidi ya hasimu wake Simba SC hapo kesho siku ya Jumamosi October 28, 2017, Bongo5 inakuletea tofauti ya timu hizi mbili kwa msimu wa mwaka 2017/18 na wachezaji Ibrahim Ajib Migomba na Emmanuel Okwi.
Sikuzote presha ya mechi ya Yanga SC dhidi ya Simba SC haizoeleki kwa zaidi ya miaka 81 sasa hii ni kuanzia kwa mashabiki,wanachama, viongozi, makocha mpaka wachezaji wenyewe.
Kuelekea katika mchezo huo mashabiki wa soka wameyaelekeza macho yao kwa wachezaji wawili wenye mvuto mkubwa kwa sasa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda na klabu ya Simba SC, Emmanuele Okwi dhidi ya Ibrahim Ajib Migomba wa Yanga SC.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ana jumla ya mabao 8 wakati Ibrahimu Ajib Migomba wa Yanga akiwa na juamla ya mabao 5.
Kutokana na mabao ya wachezaji hao, Okwi anaongoza kwa upande wa wafungaji ndani ya Simba na ligi kuu ya Tanzania Bara huku Ajib akishika nafasi ya pili.
Kutokana na mabao ya wachezaji hao, Okwi anaongoza kwa upande wa wafungaji ndani ya Simba na ligi kuu ya Tanzania Bara huku Ajib akishika nafasi ya pili.
1.Okwi amefunga mabao yote Dar es salaam katika Uwanja wa Uhuru tofauti na Ajib amabaye amefunga manne mikoani
2.Okwi amefunga nusu ya mabao yake kwenye mechi moja, Ajib ameyagawa mabao yake kwa mechi tofauti.
3. Katika kila mchezo ambao Ajib amefunga, Yanga imeshinda. Okwi amefunga katika mechi tatu tu ambazo Simba imeshinda. Kwa maana hiyo Yanga inamtegemea zaidi Ajib wa Simba haimtegemei Okwi pekee.
4. Ajib anafunga kwa kutumia miguu tu, Okwi anafunga hata kwa vichwa. Kwa mantiki hiyo Okwi ana uwezo mkubwa zaidi wa kufunga, kwa njia mbalimbali.
5. Ajibu amecheza mechi zote, Okwi amekosa mechi moja. Hii inamaanisha kuwa Okwi ana wastani mzuri wa mabao kwa idadi ya mechi alizocheza.
6. Ajib anapiga chenga, anatengeneza nafasi na magoli yake manne ameshinda nje ya 18. Okwi anacheza na nafasi, anafunga
7.Ajib magoli yake mengi anafunga kwa njia mipira ya kutenga (Set Piece Goals) tofauti na Okwi ambaye hufunga kwanjia mbalimbali.
Tofauti ya klabu ya Yanga na Simba SC kabla ya mchezo wao wa hapo kesho katika Uwanja wa Uhuru.
Klabu ya Simba itaingia uwanjani hapo kesho huku ikiwa inaongoza msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara kwa kuwa na pointi 15 sawa na Yanga anayeshika nafasi ya pili wakiwa na tofauti ya mabao 10.
Yanga SC na Simba SC hizi zote zimetoka sare zisizotarajiwa katika michezo yao ya ligi msimu huu.
Yanga imekubali kutoka sare dhidi ya Lipuli FC na Majimaji wakati mahasimu zao Simba hali ikiwa hivyo dhidi ya Mbao FC na Mtibwa Sugar.
Yanga katika michezo yake ya hivi karibuni imeonekana ikiwategemea zaidi Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa halia ambayo inaweza kuwakharimu mbele ya mahasimu zao Simba ambao hawamtegemei mchezaji mmoja katika upachikaji mabao.
Yanga katika michezo yake ya hivi karibuni imeonekana ikiwategemea zaidi Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa halia ambayo inaweza kuwakharimu mbele ya mahasimu zao Simba ambao hawamtegemei mchezaji mmoja katika upachikaji mabao.
Saikolojia katika Darby hii inaamua zaidi matokeo ya mechi mara kadhaa wachezaji wa Simba SC wanaonekana ni wenyekujiamini zaidi ukilinganisha na Yanga na hiyo hudhihirishwa na hata wingi wa mashabiki wanao kuja uwanjani ambapo mfano mzuri ni walipokutana katika ufunguzi wa msimu.
Kati ya moja ya uchambuzi wake mchezaji wa zamani wa Yanga SC, Ally Mayai amewahi kukiambia chombo cha Azam Tv, kuwa mpaka unakwisha mzunguko wa kwanza wa VPL msimu huu klabu ya Simba inatumia Kilomita alfu 8 wakiwa barabarani ikiwa ni tofauti na hasimu wake Yanga ambaye anatumia Km alfu 7 pekee.
Wanaoongoza katika orodha ya wafungaji mpaka sasa.
1. Emmnuel Okwi (Simba SC ) mabao 8
2. Ibrahim Ajib (Yanga) mabao 5
3. Mohammed Rashid (Tz Prison) mabao 4
4. Eliudi Ambokile (Mbeya City) mabao 4
1. Emmnuel Okwi (Simba SC ) mabao 8
2. Ibrahim Ajib (Yanga) mabao 5
3. Mohammed Rashid (Tz Prison) mabao 4
4. Eliudi Ambokile (Mbeya City) mabao 4
Matokeo yoyote yanayopatikana katika Darby hii huleta mtazamo hasi ama chanya kwa benchi la ufundi, walimu na wachezaji hali inayochagiza kuhatarisha nafasi za kazi zao.
Wapo baadhi ya makocha waliyotimuliwa kazi kufuatia kupata matokeo mabaya katika Darby hii na wapo wachezaji waliyo simamishwa na klabu husika kufuatia matokeo ya namna hiyo na hii inadhihrisha ukubwa wa mchezo huo wa Yanga SC na Simba SC.
Mashabiki wa timu hizi wanachohitaji ni ushindi dhidi ya mpinzani wake kuliko ubingwa wa ligi kuu.
Yanga na Simba zitashuka kesho Uwanja wa Uhuru katika mchezo wa raundi ya nane ya Vpl huku viingilio vikiwa ni shilingi 20,000 /= kwa jukwaa kuu na 10,000 kwa viti vya mzunguko.
No comments