KUELEKEA MCHEZO WA SIMBA vs YANGA, DAR DERBY, TAKWIMU ZINAONESHA LWANDAMINA NI KIBONDE KWA OMOG
Mechi ya Yanga vs Simba itakayochezwa October 28, 2017 inazalisha mechi nyingine ndani yake (yani mechi ndogo ndani ya mechi kubwa).
Leo tuanze na mechi ya makocha (George Lwandamina wa Yanga vs Joseph Omog wa Simba) ambao watakuwa na vita yao kuhakikisha mbinu zao zinaleta matokeo kwenye vikosi vyao.
Hawa wazee watakuwa wakikutana kwa mara ya nne, kabla ya hapowalishakutana katika michezo mitatu ya mashindano yote (VPL, Mapinduzi Cup na Ngao ya Jamii.)
Katika mechi zote hizo Joseph Omog anamatokeo mazuri dhidi ya Lwandamina, ameshinda mechi zote tatu walizokutana (mechi mbili kwa penati) na mchezo mmoja ameshinda ndani ya dakika 90.
Kwa mara ya kwanza Omog na Lwandamina kukutana ilikuwa ni January 10, 2017 mchezo wa nusu fainali ya Mapinduzi Cup viwani Zanzibar. Simba walishinda kwa penati 4-2 baada ya kutoka suluhu (0-0) ndani ya dakika 90.
Mara ya pili walikutana kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara tarehe 25/02/2017 Simba ikashinda 2-1 kwa magoli ya Shiza Kichuya na Laudit Mavugo, Simon Msuva alifunga goli la Yanga kwa mkwaju wa penati.
Pambano la tatu kati ya Omog na Lwandamina ilikuwa ni August 23, 2017 mchezo wa Ngao ya Jamii ambapo Simba walishinda kwa penati baada ya mechi kumalizika bila timu zote kufungana ndani ya dakika 90. Simba walishinda kwa penati 5-4.
- 10/01/2017 (Mapinduzi Cup) Simba 0-0 Yanga (Penati 4-2)
- 25/02/2017 (VPL) Simba 2-1 Yanga
- 23/08/2017 Yanga 0-0 Simba (Penati 4-5)
Jumamosi ijayo October 28, 2017 wababe hawa wataongoza wachezaji wao kutafuta matokeo kwenye mechi ya VPL, Lwandamina atakubali kunyanyaswa na Omog au atakata ‘utepe’ wa ushindi kwa mara ya kwanza dhidi ya Omog?
No comments