Jose Mourinho kuchezesha mlinzi mmoja na washambuliaji 9 dhidi ya Liverpool



Liverpool wanaikaribisha Manchester aunited siku ya Jumamosi katika uwanja wa Anfield,mchezo huu mara zote unakuwa wa upinzani mkubwa haijalishi timu zitakuwa katika viwango gani.
Kwa kipindi hiki cha sasa waandishi wengi wa habari barani Ulaya wanajaribu kutafuta habari kupitia Jose Mourinho ambaye mara nyingi hakosi cha kusema wakati wa kuelekea katika mipambano mikubwa.
Hii leo Mourinho ametoa mpya baada ya kuulizwa ni mfumo gani anaenda kuutumia katuka mchezo huu wa Jumamosi na ndipo Mourinho alipotoa jibu ambalo limekuwa kichwa cha habari kila sehemu.
Jose Mourinho aliwaambia waandishi wa habari kwamba wasiwe na shaka kwani safari hii anakwenda Anfield na mfumo mpya ambapo ataweka mlinzi mmoja huku mbele akiweka washambuliaji tisa.
Wengi wamelichukulia jibu la Mourinho kama utani lakini kwa kumbukumbu jibu hili linaonekana kama kijembe cha wale waliomponda msimu uliopita alipokwenda Anfield kwamba alienda kupaki basi.
Mourinho pia amesisitiza kwamba kusema kwamba hii ndio mechi yao ya kwanza na timu kubwa/ngumu haiwaathiri wao lakini sio sawa kwa wapinzani ambao wameshacheza nao na ni kuwashushia heshima.
Wakati huo huo Mourinho amesema Michael Carrick naye hatakuwepo katika mchezo wa kesho dhidi ya Liverpool kutokana na ugonhwa lakini mshambuliaji wao Romelu Lukaku yuko fiti kuikabili Liverpool.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.