( PICHA ) ULIPITWA NA HII YA MANARA WA SIMBA KUIWAKILISHA YANGA KUCHUKUA JEZI ZA VODACOM, HII HAPA


Wadhamini wa ligi kuu soka Tanzania Bara kampuni ya mtandao wa simu za mkononi Vodacom imekabidhi vifaa mbali mbali kwa timu zinazoshiriki msimu ujao wa mwaka 2017/18 utakao anza Agosti 26.




Vodacom imekabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 500 ambavyo ni pamoja na jezi za mazoezi na zile za mechi kwa timu zote 16 zitakazocheza ligi hiyo msimu ujao.



Wakati wa ukabiziwaji wa vifaa hivyo kwa timu mbali mbali kutoka kwa Mkurugenzi wa idara ya masoko na usambazaji Vodacom, Hisham Hendi  Msemaji wa Simba, Haji Manara ameamua kufanya masihara baada ya kuiwakilisha Yanga katika jezi hizo wakati wa hafla fupi.




Kwa kuwa hakukuwa na mwakilishi wa Yanga, Manara ambaye baba yake, Sunday Manara ameichezea timu hiyo alipanda jukwaani na kusema anawawakilisha huku akifanya utani ingawa baadhi walimpongeza na kusema aliiwakilisha timu ya baba yake, Sunday Manar



No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.