MHE. LOWASSA AHOJIWA POLISI NA KUACHIWA KWA DHAMANA BAAADA YA MASAA MANNE (4)

Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Edward Lowassa ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa saa manne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) leo jijini Dar es salaam.




Akizungumza na waandishi wa Habari mapema baada ya mahojiano hayo Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Kibatala amesema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi ya wiki hii saa 6.00 mchana.
Kibatala amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
Mzee amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23, mwaka huu wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa ameandika Maelezo ya Onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29,” amesema Kibatala.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.