MAMBO USIO YAJUA KUHUSU MBUGA ZA WANYAMA TANZANIA
Na
Jumia Travel Tanzania
Inastaajabisha
kuona watu wa mataifa ya nje wanajua vitu vingi zaidi vinavyopatikana Tanzania
kuliko watanzania wenyewe. Sijui ni ile hulka ya kutopenda kufuatilia mambo au
ni dhana kwamba waache wageni waje kushangaa maana hivyo vitu vitaendelea
kuwepo tu.
Nchi
yetu imebarikiwa na inaendelea kubarikiwa kugunduliwa kwa mambo mengi zaidi ya
kustaajabisha ambayo hayapatikani kwingineko duniani. Jumia Travel ingependa
kukufumbua macho kwamba yafuatayo ni baadhi tu ya mambo yanayopatikana na
unaweza kuyashuhudia ukiwa nchini Tanzania.
Mti
mrefu zaidi barani Afrika. Hivi karibuni mtafiti kutokea Chuo Kikuu cha Byreuth
cha nchini Ujerumani, Dkt. Andreas Hemp baada ya utafiti wa takribani miaka 20
amethibitisha kuwa Tanzania ina mti mrefu zaidi kuliko yote barani Afrika ukiwa
na urefu wa mita 81.5. Mti huo kwa jina la kitaalamu unajulikana kama
‘Entandrophragmaexcelsum’, ni aina adimu sana ya miti na inaweza kuwa na umri
wa zaidi ya miaka 600. Ili kuweza kuuona mti huo unaopatikana katika safu ya
misitu ya Mlima Kilimanjaro na kuwa kivutio kikubwa kwa watalii hivi sasa,
itakupasa utembee umbali wa masaa 2.30 mpaka kutokea kijiji cha Tema ili
kuufikia.
Twiga
mweupe aonekana kwa mara ya kwanza.
kubisha kwamba hiko kitu hakiwezekani
lakini ndio maajabu ya Mungu hayo, twiga mweupe ameonekana Tanzania. Takribani
mwaka mmoja uliopita, mwanzilishi na mwanasayansi katika Taasisi ya Misitu
Asilia katika hifadhi ya taifa ya Tarangire inayopatikana mkoani Manyara, Dkt.
Derek Lee alimuona twiga mwenye rangi nyeupe. Twiga huyo ambaye alikuwa na umri
wa miezi 15 amepewa jina la ‘OMO,’ rangi yake inaonekana kama vile imechubuliwa
tofauti na rangi asilia ya twiga tunaowajua. Mtafiti huyo amesema kuwa twiga
huyo anasumbuliwa na ‘leucism,’ ni hali inayosababisha kupotea kwa baadhi ya
rangi. Licha ya utofauti huo na wenzake lakini bado mnyama huyo anajichanganya
na wengine na wenzie kutojali utofauti huo kabisa.
Asilimia
30% ya ardhi ya Tanzania ni hifadhi za wanyama pori. Kama ulikuwa haujui basi
ni kwamba nchi ya Tanzania sehemu ya asilimia 30 ya ardhi yake ni hifadhi za
wanyama pori wa aina mbalimbali duniani. Tanzania inazo hifadhi za taifa 16
ambazo zinasimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ambapo kwa
ujumla wake zina ukubwa wa kilometa za mraba takribani 42,000. Kwa mfano,
hifadhi ya taifa ya mbuga ya Serengeti ni mojawapo ya mbuga maarufu na
inayopendwa zaidi duniani, ni makazi ya aina mbalimbali za wanyama zaidi ya
milioni moja. Pia imetangazwa kuwa ni Eneo la Urithi wa Dunia na kutajwa
mojawapo ya sehemu ya Maajabu Saba ya Dunia.
Takribani
wanyama milioni 2 hushiriki tukio la kuhama linalotokea kila mwaka mbuga ya
Serengeti. Kila mwaka watalii hushuhudia tukio la kipekee la uhamaji wa makundi
ya wanyama wa aina ya pundamilia na nyumbu zaidi ya milioni 1.5. Tukio hilo
hutokea kati ya Kusini mwa bonde la mbuga ya Serengeti nchini Tanzania kuelekea
eneo la Kaskazini mwa mbuga ya Masai Mara iliyopo Kenya. Lengo kubwa la tukio
hilo ni katika harakati za kutafuta malisho mazuri kwa wanyama hao ambalo
hutukia mnamo miezi ya Mei mpaka Desemba ingawa muda huwa unaweza kubadilika.
Sehemu inayosisimua zaidi ni pale wanyama hao wanakatisha mto Mara kuuvuka
kuelekea Masai Mara, wanyama hao kwa makundi na ujasiri mkubwa huvuka licha ya
kuwa na mamba wakali.
Mbuyu
unaweza kuishi mpaka miaka 1,000. Mibuyu ni miti mikubwa na inayovutia zaidi,
hapa nchini Tanzania unaweza kuiona vizuri zaidi ukitembelea hifadhi ya taifa
ya Tarangire. Kama ulikuwa haufahamu ni kwamba baadhi ya aina ya miti ya mibuyu
huweza kuishi kwa takribani miaka 1,000 au zaidi. Inasemekana mbuyu mkongwe
zaidi unapatikana nchini Afrika ya Kusini ni unaaminika kuwa na miaka takribani
6,000.
Uwepo
wa vitu hivyo Tanzania ni uthibitisho wa namna nchi hii ilivyobarikiwa na
vivutio mbalimbali ambavyo watu wengi hawavifahamu bado. Kwa hayo machache
Jumia Travel inaamini utakuwa umejifunza na kupata shauku ya kutembelea maeneo
hayo pamoja na kukuongezea ari ya kujifunza mengineyo zaidi.
No comments