Baada ya Lioneil Messi na Cr7, hawa wafuatao wanaweza kuchukua nafasi zao

 Habari kubwa katika soka kama habari ya Cristiano Ronaldo kubeba tuzo yake ya 5 ya Ballon D’Or, Cr7 na Lioneil Messi ni wazi kwamba muda wao wa kuwa bora duniani unaelekea ukingoni kwa sasa lakini wafuatao wanaweza kuchukua nafasi zao.


1.Neymar. Huyu ndio anapewa nafasi kubwa zaidi kuchukua utemi wa Cr7 na Messi katika soka, tangu ahamie PSG jina lake limekuwa likizungumzwa sana na wachambuzi wakubwa wa soka akiwemo Shaffih Dauda wanampa nafasi kuwa mfalme wa soka.


2.Kylian Mbappe. Kama ilivyo kwa Neymar, huyu naye anapewa nafasi kuwa mwanasoka bora wa dunia, lakini tatizo kubwa ambalo naliona kwa Mbappe ni kivuli cha Neymar kwani kwa sasas hata uwe na uwezo vipi lakini ukiitaja PSG jina linalotajwa ni Neymar.
3.Harry Kane. Nani mshambuliaji hatari zaidi duniani kwa sasa? Sina uhakika wa moja kwa moja ni nani lakini kwa mawazo ya harakaharaka Harry Kane ni kati ya tishio kubwa kwa sasa ulimwenguni, sio rahisi sana kuwa mchezaji bora wa dunia ukiwa Tottenham lakini bado ana nafasi.
4.Eden Hazard. Amekuwa imara sana na kati ya vipaji vikubwa sana katika soka kwa sasa lakini Chelsea sio kubwa kiasi cha kumpa Ballon D’Or, kama akihamia klabu ambayo inaweza kuchukua Champions League mara nyingi itamuweka katika eneo zuri kuwa mkubwa zaidi.
5.Paulo Dyabala. Anatajwa kama Messi mpya ndani ya Argentina na raia wenginwa Argentina wana imani kubwa naye, wakati huu ambao Messi umri wake unakwenda ni wazi kwamba itampa wigo mpana zaidi wa kuwa mchezaji mkubwa zaidi.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.