VIDEO:: CHELSEA WAFANYIWA 'UNYAMA' MKUBWA NA WATFORD BAADA YA MIAKA 22.



Haina ubishi kwamba kwa sasa kati ya makocha wenye vibarua vigumu hivi sasa ni Antonio Conte, kipigo usiku wa leo mbele ya Watford kinaweza kuwa hitimisho la uvumilivu wa Roman Abromovich.
Chelsea waliokuwa pungufu walianza kutungulia dakika ya 42 ya mchezo kwa goli la penati la Troy Deeney ambaye sasa anakuwa amefunga penati sawa na Harry Kane na Kun Aguero (12) katika EPL tangu 2015.

Dakika ya 82 Eden Hazard aliisawazishia Chelsea waliokuwa pungufu baada ya Tiemoue Bakayoko kuoneshwa kadi nyekundu na kuonekana kama mpira utaisha kwa suluhu lakini dakika 2 baadae Daryl Janmaat aliongeza bao la 2 kwa upande wa Watford




Zikiwa zimesalia dakika 2 kwa mchezo kumalizika Gerard Deulofeu aliwaandikia Watford bao la 3 na kabla ya Roberto Pereyra kuandika la 4, na kwa mara ga kwanza Chelsea anafungwa mabao 4 katika EPL tangia mwaka 2015.

Kama ulikuwa hujui tu ni kwamba mara ya mwisho kwa Chelsea kupoteza michezo miwili kwa mabao 3+ ilikuwa miaka 22 iliyopita na kipigo cha hii leo kinafanya jambo hilo kujirudia tena.

BOFYA HAPA KUONA MABAO YOTE YA WATFORD VS CHELSEA




MSIMAMO WA EPL BAADA YA MCHEZO WA JANA



No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.