UTAFITI:: WANASAYANSI WADAI CHAI YA MOTO YAWEZA KUSABABISHA SARATANI YA KOO



Wanasayansi nchini China wamefanya utafiti na kugundua kuwa unywaji wa chai ya moto mara kwa mara unaweza kusababisha saratani ya koo.

Kwa mujibu wa makala iliyochapishwa katika jarida la Annals of Medicine Internal, hali ya afya na tabia ya kula ya watu 456,155 kati ya umri wa miaka 30-79 ilichunguzwa wakati wa utafiti huo.

Utafiti umefanywa ndani ya miaka kumi.

Imebainika kuwa watu amabo hunywa mara kwa mara chai ya moto au gramu 15 za pombe wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata saratani ya koo,mara tano zaidi ya asiyekunywa.

Na kwa wavuta sigara,kuna uwezekano wa wao kupata ugonjwa huo mara mbili ya mtu asiyevuta sigara.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.