NJIA 7 ZA KUWA MAFANYABIASHARA MKUBWA
1. Chagua wazo bora la kibiashara.
Wazo bora la kibiashara ndilo litakalo kufanya kuwa mfanyabiashara wa mkubwa. Mara nyingi nimekuwa nikikutana na watu wakisema wanataka kuwa wafanyabiashara na kuishia kusema tu. Ila ukweli ni kwamba katika kuchagua wazo bora la kibiashara ni lazima ujiulize je unataka kuwa mzalishaji wa bidhaa au huduma? Je unataka kuwa mnunuzi na muuzaji?au je unataka kuwa msambazaji tu ? Hayo yanaweza kuwa miongoni mwa maswali ya msingi ya kujiuliza.
2. Fanya uchunguzi juu ya washindani wako.
Hapa ndipo jicho la tatu linaposhindwa kufanya kazi mara nyingi. Tumekuwa si wachunguzaji wazuri juu ya washindani wetu ila tumekuwa wasikilizaji tu kwa watu wengine juu ya washindani wetu. Ila ikumbukwe ya kwamba fanya uchunguzi wa kutosha ili kujua washindani wako wanatumia mbinu zipi kukuza biashara zao. Hii itakusadia pia kujua ni wapi wanapokosea ili uweze kulizipa pengo hilo. Kwa kufanya hivi kutakufanya ndoto zako za kuwa mfanyabiashara wa kimataifa zitimie.
3. Tafuta mtu wa kukuongoza. (Helpful mental).
Tafuta mtu sahihi wa kukuongoza na si mtu wa kukukwamisha. Watu wengi tunashindwa kuwa wafanyabishara wakubwa hii ni kutokana tunatafu watu ambao sio sahihi katika kutushauri. Stuka mapema juu ya jambo hili. Na anza kukaa na watu ambao tayari wamefanikiwa kwenye biashara zao watakusaidia sana kufika kule unakotaka kufika kibiashara. Siku zote ukitaka kuruka kama tai, ni lazima ujifunze kama tai wanavyoruka. Kwa maana huyo ukitaka kuwa mfanyabiashara mkubwa kubali kuchukua mwongozo wa wafanyabiashara waliofanikiwa.
4. Tambua biashara inayokua.
Ukilijua hili ni jambo jema zaidi. Moja ya tatizo kubwa ni kwamba tumekuwa tukishuhudia biashara hazikuwi miaka nenda miaka rudi. Hii ni sababu kubwa ambayo inachangia tusiweze kujua ni kwa jinsi gani tusiwe wafanyabiashara wakubwa. Natamani kuona malengo yako yanabadilishwa kila wakati. Kwa mfano leo unauza nguo kwa kutembeza, ili kuona biashara inakuwa tunataka kuona unapata chumba kwa ajili ya kufanyia biashara hiyo napo kweli tunasema biashara inakua. Kama unafanya biashara mkoa wako mzima tunatamani kuona unaongeza mkoa mwingine na mwingine katika kusambaza huduma au bidhaa.
5. Panga malengo na mipango ya biashara yako.
Hapa inahusiana na juu ya kuuza, kununua bidhaa au huduma. Lazima malengo ya biashara yako uyapange kila robo ya mwaka ili kugundua kama biashara yako inakuwa au haikui. Na lazima pia katika kupanga malengo yako, utambue baada ya muda fulani biashara yako itakuwa imefika wapi. Kwa mfano ni muhimu kujua biashara yako itakapokuwa baada ya miaka miwili au mitatu mbeleni.
6. Tangaza biashara yako.
Wateja wako ni lazima wajue bidhaa na huduma ambayo unazalisha. Si kujua tu, lengo jingine la kutangaza bidhaa au huduma inamfanya mtumiaji aweze kujua jinsi ya kutumia kitu hicho. Kwa kutangaza biashara wateja huongezeka kwa asilimia kubwa sana na kufanya huduma au bidhaa yako kuweza kupendwa na wengi pia. Matangazo ni njia mojawapo bora ya kukufanya kuwa mfanyabiashara wa kimataifa ikiwa utaitumia vizuri.
7. Jenga mahusiano mazuri na wateja wako.
Jitahidi kulizingatia hili ya kwamba Kauli katika biashara ni mali kuliko hata pesa. Jali wateja wako na kuwafanya wajihisi kama wanapata bidhaa bure. Kwa kadri utakavyozidi kujenga mahusiano bora na wateja hiyo itapelekea wao kupenda bidhaa zako na hiyo itakusaidia kukuza wateja wengi siku hadi siku.
Ni matumaini yangu umenielewa vizuri hizo ni baadhi ya siri chache kati nyingi zitakazokufanya kuwa mfanyabiashara mkubwa. Asante sana na usisite kumshirikisha mwingine.
No comments