MESSI AFUNGA KWA MARA KWANZA "DARAJANI" HUKU BAYERN "IKIUA" ZA KUTOSHA




Kabla ya jana, Lionel Messi alikuwa hajawahi kuwafunga Chelsea katika michezo 8 iliyopita ambayo waliwahi kukutana, pamoja na mabao 595 aliyokuwa nayo hakukua na bao vs Chelsea.
Lakini usiku wa jana Lionel Messi amefuta mkosi huo baada ya kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Chelsea japo bao lake lilikuwa la kusawazisha baada ya Chelsea kutangulia kupitia Willian.



Bao la leo la Willian lilikuwa bao lake la 9 katika klabu bingwa Ulaya(muda wote) na sasa anakuwa amefunga mabao 6 kati ya hayo nje ya box huku Messi sasa anakuwa na jumla ya mabao 18 vs timu za Uingereza.
Bayern Munich wakiwa nyumbani walishusha kipigo cha mbwa mwizi kwa Bestikas waliokuwa pungufu baada ya Domagoj Vida kupewa kadi nyekundu dakika ya 16 na kuwachapa bao 5 kwa nunge.


Mabao kutoka kwa Thomas Mueller(2), Roberto Lewandoski(2) na Kingsley Koman yanawafanya Bayern kufikia rekodi yao ya mwaka 1980 ya kucheza michezo 14 ya mashindano tofauti na kushinda yote mfululizo.





No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.