MBINU BORA YA KUISHI NDANI YA BAJETI YAKO
Nasema hivi kwa sababu moja kati ya tabia ya watu wengi huwa wanaishi nje ya bajeti ambayo wanakuwa wamepanga.
Yote hii hutoka na sababu kubwa moja, sababu hiyo ni pale mtu ambapo amepata fedha nyingi kwa wakati mmoja. Kitendo hicho ndicho ambacho humfanya mtu kuweza kuishi nje ya bajeti yake ya kila siku.
Kwa mfano mtu akipokea mshahara hawezi kuishi maisha ambayo alikuwa ameyazoea ukifananisha na alipokuwa hana pesa, unakuta matumizi yanakuwa mengi kuliko pesa aliyonayo. Wapo wengine mara baada ya kutumia pesa yote hujikuta wanaingia kwenye madeni yasiyo ya msingi.
Achilia mbali madeni, wapo baadhi ya watu pindi wapatapo pesa utakuta wananua vitu vingi hata ambavyo hawakupanga kununua, tatizo hili lipo kwa watu wengi sana, siwezi ita tu ni tatizo bali ni ugonjwa wa matumizi ya pesa.
Niliwahi soma kitabu kimoja cha kanuni ya pesa, ndani ya kitabu hicho mwandishi anasema ya kwamba ukimpa mtu maskini pesa basi ndani ya sekunde kadhaa basi jiandae kujua tabia za mtu huyo, hii ni kwasababu ni mtu ambaye mara zote huongozwa na pesa, basi kila kilichopo mbele yake anataka kukimiliki yeye.
Lakini pesa hiyo ukimpa mtu ambaye anaelewa ni nini maana ya pesa, basi pesa hiyo huweza kufanya kitendo cha uwekezaji, ili pesa hiyo iweze kujizalisha yenyewe hapo baadae. Kwa nukta hiyo jaribu kutafakari hivi pesa ambayo huwa unaipata mikononi mwako unajiona upo kundi gani kati ya hayo niliyoyaeleza?
Kama utaona ya kwamba upo kundi ambalo umekuwa ni mtumiaji mzuri kuliko kuwa mwekezaji basi tambua lipo tatizo kubwa ndani yako, ambalo linakufanya uishi nje ya mstari wa bajeti yako, Hivyo unatakiwa kujua ni kwa namna gani unatakiwa kuishi ndani mstari bajeti yako kwa kuzingatia jambo hili.
Jambo Kwanza kabisa hakikisha pesa isikupelekeshe hasa pale unapoipata ila wewe ndiyo unatakiwa kuipelekesha pesa, kwa kuzingatia ya kwamba pindi utakapo ipa nafasi pesa ikuendeshe basi tambua fika lolote linaweza kutokea ndani yako.
Lakini pia kwa kuwa wanasema pesa ina makelele sana hasa pale unapoipata hivyo hakikisha pale unapoipata pesa unaishi kwenye pajeti yako ambayo umeizoa, kwani pindi utapopandisha bajeti yako eti kwa sababu umeipata pesa basi tambua ya kwamba utaunganaa na wale wanaosema vyuma vimekaza.
Hivyo pesa isiongeze matumizi yako ya kila siku eti kwa sababu umepata pesa, hivyo kila wakati jifunze kuishi ndani ya bajeti yako.
No comments