MAN U, CHELSEA ZACHEZEA VIPIGO JANA, CITY WAZIDI KUJICHIMBIA, TAZAMA HAPA MATOKEO YOTE YA EPL JANA.


Christian Eriksen alifunga bao sekunde ya 11 tu ya mchezo, bao la Eriksen ndio linakuwa bao la mapema zaidi kwa Manchester United kuwahi kufungwa katika ligi kuu ya EPL
.

Lakini mlinzi wa Manchester United Phill Jines akijifunga bao lililoufanya mchezo kuisha kwa Tot kushinda kwa bao 2 kwa 0 na sasa Tot wanakuwa wamefaidika kwa mabao 3 ya kujifunga ndani ya msimu huu.

Ushindi wa jana usiku wa Tottenham mbele ya United unawafanya Tottenham Hotspur kwa mara ya kwanza baada ya miaka 52 iliyopita kuwafunga Manchester United katika michezo mitatu nyumbani kwao.

Mchezaji mpya wa Everton Theo Walcotta lifunga mara mbili wakati Everton ikiichapa Leicester bao 2 kwa 0 huku Chelsea wakiwa nyumbani wakakubali kipigo cha mabao 3 kwa nunge toka kwa Afc Bournamouth.



Newcastle wakiwa nyumbani walilazimishwa suluhu ya bao moja kwa moja dhidi Burnley, Stoke City na Watford nao wakamaliza mchezo wao kwa sare ya kutokufungana.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.