KUMBUKA KUWA OKWI, BOCCO, NDIO WACHEZAJI WALIOFUNGA MAGOLI MENGI ZAIDI YA TIMU 14 VPL


Wakai mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara ukiwa umemalizika kwa kila timu kucheza mechi 15, washambuliaji wawili wa Simba wamefunga idadi kubwa ya magoli kuliko timu 14 na wamezidiwa goli moja tu na mabingwa watetezi Yanga.
Emanuel Okwi na John Bocco kwa pamoja wamefunga jumla ya mabao 19, Okwi akiwa amefunga magoli 12 na John Bocco amezama kambani mara saba (7). Ida hiyo ya magoli inawafanya kuwa wachezaji wenyenmabao mengi kuliko baadhi ya vilabu na kuzidiwa goli moja na Yanga ambayo imefunga jumla ya magoli 20 katika mzunguko wa kwanza.
Okwi ndiye anaongoza chati ya wachezaji wenyebmagoli lakini magoli yake yote akifunga kwenye viwanja viwili tu, Uhuru na uwanja wa Taifa. Raia huyo wa Uganda amefunga magoli 12 katika mechi sita alizocheza katika viwanja hivyo.
Simba ndio timu yenye magoli mengi ya kufunga katika mechi 15 zilizopita, imefunga magoli 35 ikiwa imeruhusu magoli sita kwa mechi ilizocheza mzunguko wa kwanza.
  • Timu zinazozidiwa magoli na pacha inayoundwa na Bocco na Okwi ni pamoja na Azam FC (16), Singida United (14), Mtibwa Sugar (11), Tanzania Prisons (15), Lipuli FC (8), Ndanda FC (9), Mbao (14), Mwadui (14), Mbeya City (12), Ruvu Shooting (9), Kagera Sugar (7), Majimaji (12), Njombe Mji (8), Stand United (5).
Okwi pekeyake ana vizidi magoli vilabu saba (Mtibwa Sugar, Lipuli, Ndanda, Ruvu Shooting, Kagera Sugar, Njombe Mji na Stand United).

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.