DAKIKA 7 ZILITOSHA KUIANGAMIZA KABISA PSG, CR7 HASHIKIKI UEFA, LIVERPOOL NJIA NYEUPE



Mtoto yake nepi” Real Madrid wamedhihirisha msemo baada ya usiku wa leo kutoka nyuma kwa bao 1 kwa 0 mbele ya PSG na kisha kuumaliza mchezo huo kwa ushindi wa mabao 3 kwa 1.
Cristiano Ronaldo alikuwa shujaa wa Real Madrid baada ya kuweka kambani mabao mawili ambapo sasa nakuwa na mabao 116 na ni timu 19 tu katika Champions League ndio zimefunga mabao mengi zaidi yake.


Liverpool nao waliangusha kipigo cha mbwa mwizi kwa Fc Porto baada ya kuwapiga mkono(mabao 5) huku utatu wa Sadio Mane, Mohamed Salah na Roberto Firminho ukiendelea kuwa cancer kwa wapinzani.


Sadio Mane alifunga mabao 3 na kumfanya kuwa mchezaji wa 3 kwa Liverpool kufunga hattrick chini ya Jurgen Klopp baada ya hattrick za Divick Origi (Dec 2015) na ile ya Phillipe Coutinho(2007).


No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.