BOCCO KUSAFIRI NA SIMBA KUELEKEA DJIBOUTI.


Mshambuliaji John Bocco ameonekana hajaumia sana kiasi cha kulazimika kukaa nje ya uwanja.

Baada ya vipimo alivyofanyiwa kutokana na maumivu aliyoyapata katika mechi dhidi ya Mwadui FC, Bocco ataweza kusafiri na Simba kwenda Djibouti.

Simba inakwenda Djibouti kuwavaa Gendamarie katika mechi ya pili ya Ligi ya Kombe la Shirikisho.

Katika mechi ya kwanza, Simba imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Vipimo vimeonyesha ameumia lakini si kiasi ambacho kitamzuia kuendelea na majukumu yake. Ameshaanza kupata matibabu na ataungana na wenzake hata safari ya Djibouti,” kilieleza chanzo.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.