YAJUE MAMBO AMBAYO HUTAKIWI KUFANYA KABLA YA KULALA

 


Ni vyema kujifunza tabia njema zitakazokuwezesha upate usingizi bora unaouhitaji na kuamka ukiwa umechangamka na kuwa tayari kukabiliana na siku. Usipopata walau masaa saba au tisa ya usingizi kila siku, unajiweka kwenye hatari ya kuvurunda kazini, uchovu na wakati mwingine hata kupata ajali.






Kwa mujibu wa kamisheni ya utafiti wa matatizo ya usingizi nchini Marekani, matatizo hayo husababisha hasara za moja kwa moja ifikayo dola milioni 15.9 na yasiyo ya moja kwa moja, dola bilioni 50 hadi 100 kila mwaka.


Matatizo hayo husababisha ajali nchini humo zifikazo 100,000, majeruhi 71,000 na vifo 1,550. Hakuna takwimu za uhakika za Tanzania lakini ajali nyingi pia zinazotokea nchini, zipo zilizotokana na dereva kusinzia akiwa kwenye usukani.
Hizi ni tabia tatu za kuepuka:


1. Kutumia teknolojia kitandani
Usiipeleke smartphone yako, iPad au kifaa kingine cha teknolojia kitandani. Itakuwa ngumu kupata usingizi ukifanya hivi. Kwa kawaida si rahisi kuepuka hili sababu watu wengi sasa hupanda kitandani na simu zao na kuchat hadi muda wanapoamua kulala lakini hii ni tabia mbaya na yenye athari. Ni muda wa kuipunguza kama unataka kupata usingizi bora. Wataalam wanasema ni vyema kuepukana na electronics walau saa moja kabla ya kwenda kulala.





2. Kutumia vinywaji vyenye kahawa
Kahawa inafahamika vyema kwa jinsi inavyokata usingizi na kama unakumbuka shuleni watu hutumia sana kama wanataka kujisomea. Hivyo kama unataka kukesha ukiangalia ceiling usiku kucha, unaweza kuchukua kikombe cha kahawa na kunywa. Caffeine huingia kwenye njia ya damu kupitia tumbo na utumbo mwembamba na huanza kufanya kazi dakika 15 tu baada ya kuinywa. Inapokuwa tumboni, hufanya kazi kwa masaa kibao.


3. Mazoezi
Mazoezi mazito huleta ugumu kwa baadhi ya watu kulala. Awali ilikuwa ikidaiwa kuwa watu wote wanatakiwa kuepuka kufanya mazoezi kabla ya kulala. Lakini utafiti mpya umebaini kuwa hii si kweli kwa kila mtu. Lakini kama upo kwenye kundi la wanaoathirika ni vyema ukasubiri hadi asubuhi. Kama unapenda mazoezi jioni ni muhimu kufanya masaa machache kabla ya muda wa kulala. Hii itaupa mwili wako muda wa kutosha kupumzika.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.