WCB: DIAMOND ATOA KALI YA MWAKA KATIKA HARUSI YA SHILOLE, HARMONIZE ATOA GARI YA 9M

Msanii wa muziki, Harmonize alihudhuria sherehe ya ndoa ya Shilole na Uchebe, ambapo ametoa zawadi ya tsh milioni 9 kwaajili ya kununua gari aina ya Noah ili liwasaidie wawili hao katika shunguli zao biashara. Muimbaji huyo wa WCB aliambatana na mpenzi wake, Sarah.





mbali na hiyo ya Harmonize Rais wa WCB, Diamond Platnumz alitoa kali ya mwaka katika sherehe ya harusi ya Shilole na Uchebe baada ya kumtaka bibi harusi huyo kuchagua zawadi ambayo anaitaka kutoka kwake. Baada ya Diamond kusema hivyo, Shishi alimuomba muimbaji huyo kujitolea kumtangazia biashara yake mpya ya Shishi Chili, ambapo Diamond alikubali ombi hilo.






Jux na Vanessa hawakua nyuma nao,

Kila msanii aliyehudhuria harusi ya Shilole na Uchebe alitoa zawadi ya aina yake kwa wawili hao, Jux alisema yeye anachofanya kama zawadi kwa Shilole ni kumsomesha mtoto wake moja kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo pia mpenzi wake Vee Money alisema atamlipia muimbaji huyo kulala katika hotel ya nyota tano ya Kilimanjaro.





No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.