TOFAUTI YA MAN U NA YEOVIL ILIVYO TESWA NA SANCHEZ AKITOA 'ASSIST' YAKE YA KWANZA UNITED



Manchester United wamefudhu kwa hatua ijayo ya michuano ya FA baada ya kuipiga Yeovil Town mabao 4 kwa nunge huku Alexis Sanchez akiibuka mchezaji bora wa mechi hiyo na akimaliza mchezo na assist 1.



Lakini Yeovil Town ni wanyonge sana yaani wanyonge mno mbele ya United, uwanja wao tu wa Hunish Park unapokea mashabiki 9,527 wakati uwanja wa Manchester United unapokea mashabiki 74,994.
Kubwa zaidi pesa ambayo Alexis Sanchez anapeleka nyumbani kila wiki ni £350,000 lakini kwa ujumla wachezaji wa Yeovil Town kila mwisho wa wiki pesa wanayoipata kwa ujumla ni £23,000.
Wakati Manchester United wana usajili mmoja ambao umewagharimu kiasi cha £89m, Yeovil Town wao usajili wao wa ghali zaidi unatajwa kuwa ulikuwa wa £250,000 na hiyo ndio rekodi yao kubwa kabisa ya usajili.


Viwango vya mishahara kwa ujumla kwa wachezaji wa Manchester United inatajwa kuwa £265.5m lakini Yeovil Town wenyewe kiwango chao kwa ujumla kwa timu nzima inakadiriwa kuwa ni £1.2m.





No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.