SABABU ZA SIMBA KUKIMBILIA MOROGORO KUJIWINDA NA SINGIDA UNITED



Kume kitu kikubwa ambacho Simba walikuwa wanakifanyia mazoezi mkoani Morogoro ni suala la ufungaji magoli, kaimu kocha mkuu wa timu hiyo Masoud Djuma amesema ushambuliaji ndio sehemu ambayo ameifanyia kazi kubwa wakiwa kambini.
Masoud amesema, timu inacheza vizuri na kufika hadi goli la timu pinzani lakini kikwako kikubwa kimekuwa ni utulivu na kupasia nyavu hivyo wamefanya mazoezi ya kutosha katika eneo hilo kuelekea mchezo wao wa ligi dhidi ya Singida United.
“Ushambuliaji, timu inacheza tunafika mbele ya goli lakini utulivu mbele ya goli na kumalizia ndio ilikuwa shida. Kama unafika mbele ya goli mara nyingi halafu nafasi hauzitumii lazima tu utafungwa, tuliongea sana na wachezaji kuhusu hilo na tumefanya mazoezi nafikiri mungu atasaidia mambo yatakuwa vizuri.”
“Kitu kingine kilichonivutia Morogoro ni uwanja ulivyo mkubwa huenda ukalingana na tutakaoutumia kwenye mechi, tulipata mechi na timu mbili kuona kila mtu anaweza kutusaidia vipi.”
“Kutoka mjini kumetusaidia kwa sababu tulitoka kwenye wakati mgumu wa kutolewa kwenye Mapinduzi Cup ilikuwa ni lazima tupate sehemu ya kutulia ili tuachane na habari za watu kuhusu Mapinduzi.”
Kuhusu mchezo dhidi ya Singida United
“Mchezo ni mgumu ndio maana viongozi walifikiria kuitoa timu mjini kuipeleka Morogoro ambako kuna hali ya hewa nzuri uwanja mzuri, nafikiri kwa mwalimu yeyote kupta pitch kama ile inakupa uhuru wa kuwapa wachezaji mazoezi yoyote unayotaka.”
Hali za wachezaji kuelekea mchezo
“Hakuna majeruhi labda Haruna Niyonzima ambaye hayupo, wengine wote wanaweza wakacheza.”
Tetesi kuhusu niyonzima kukaa nje kwa muda mrefu
“Mimi kama kocha nafikiri hiyo sio kazi yangu ni kazi ya daktari, nimeongea na haruna asubuhi ameniambia anaenda kupata vipimo vya mwisho hospitali akasema atanijulisha lakini kwa sasa sina jibu.”
Mchezo utakuwa wa aina gani?
“Tunalazimika kufunga kwa sababu tunahitaji ushindi kuliko wao labda, kulingana na nafasi ambayo tupo, wao wanaweza kuhangaika na fa cup sisi nafasi hiyo hatuna.”

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.