NDEMLA APEWA ZAWADI YA GARI NA HANS POPPE BAADA YA KUONESHA KIWANGO KIZURI DHIDI YA SINGIDA UNITED




January 18-2018 klabu ya Simba ilifanikiwa kuidhibu klabu ya Singida United goli 4-0 ikiwa ni kipigo kikubwa kwa kocha mkuu wa Singida United Hans Van Der Prjium tangu aanze kukinoa kikosi hicho.

 Magoli yaliyoiua Singida yalifungwa na kijana machachari Shiza Kichuya, Asante Kwasi na Emmanuel Okwi aliyefunga mawili. Baada ya mchezo huo mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Simba Zancharia Hans Poppe alitoa zawadi ya gari kwa Said Hams Ndemla.

 Kiwango alichokionesha Ndemla katika mchezo huo dhidi ya Singida kilimshawishi mwenyekiti huyo wa Usajili na kutangaza kumpa zawadi ya gari Said Ndemla. Katika ushindi huo magoli mawili yaliyofungwa na Emmanuel Okwi na Asante Kwasi yalitengenezwa na Said Ndemla. 




Hans Poppe alisema kuwa yalikuwa amfatilia Ndemla kwa muda mrefu huku akiangalia mchezaji mwenye nidhamu na yule asiyeweza kubadilika, ndipo alipomuona Ndemla. Aliongeza na kusema Ndemla amekuwa akianzia benchi lakini akiingia uwanjani anaonesha kiwango cha aina yake, tena Ndemla hakuwahi kuonesha utovu wa nidhamu pamoja na kukaa benchi.

 Pamoja na zawadi ya gari Ndemla aliibuka SimbaApp Man of the Match kwenye mchezo wa huo dhidi ya Singida United. Pichani ni Ndemla akishangilia pamoja na kimara wa magoli Emmanuel Okwi ambapo jana alitimiza magoli 10 kwenye Msimu huu 2017/18. 






No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.