HIZI NDIZO FAIDA ZA KULIA


Mtafiti wa machozi Bergman anasema, "Kuzuia machozi huongeza viwango vya shida, na huchangia magonjwa yaliyotokana na matatizo, kama shinikizo la damu, matatizo ya moyo, na vidonda vya peptic.

MACHOZI ni njia ya asili ya kuongea hisia za moja kwa moja kutoka moyoni lakini pia machozi ni njia ya kuongea vitu vingi kwa wakati mmoja.

TAFITI tofauti tofauti zilizofanyika zinaonyesha wanawake kati ya asilimia 85 wanakiri kwamba baada ya kutoa machozi au kulia wanajisikia ahueni, raha na wanakuwa 'relaxed'.

Kuna aina tatu za machozi ya binadamu

1. Emotional Tears: Haya ni machozi  ambayo hutoka kutokana na kuguswa hisia, au kuumizwa moyoni.

2. Basal Tears: Haya ni machozi ambayo hufanya macho yetu kuwa na majimaji kila wakati ( lubiricating tears) na kufanya macho yaone vizuri.

3. Reflex Tears: Ni machozi ambayo huweza kutoka pale kitu kinachowasha macho kuingia machoni kama vile kitunguu, mabomu ya machozi nk.


Faida za kutoa machozi

Machozi hutoa sumu: Hii ni kwa mujibu wa Biochemist William Frey, ambaye ni mtafiti wa machozi anasema machozi huondoa sumu kutoka  mwilini.

Machozi huonesha uwazi na hutoa hisia za moyoni.

Kuondoa Stress; Wataalamu wanasema machozi yana kiwango kikubwa cha madini ya Manganese na homoni za prolactin ambazo husaidia mliaji kujisikia ahueni baada ya kumaliza kulia.
Kutoa machozi husaidia mwili  kuondoa  kemikali, Unapotoa machozi ukiwa na hisia mwili huweza kutoa homoni za protein kama vile 'Leucine Enkephalin', hupunguza stress zaidi na kukufanya ujisikie raha na haueni.


Njia nzuri ya kulia au kutoa machozi,
Wataalamu wanashauri ukiona una stress, umekarisika ,umeumizwa ,una mawazo au unajisikia kulia au kutoa machozi , tafuta sehemu ambayo ni tulivu na ya siri (inaweza kuwa chumbani ukajifungia) peke yako, kisha ruhusu kilio ambacho machozi yanayotiririka yenyewe hadi chini kwenye mashavu, pia  hakikisha unaruhusu hisia zako za ndani zihusike na kulia kwako itakuwa ni tiba bora zaidi na utajisikia vizuri zaidi baada ya kulia.


Angalizo
Usimzuie mtu kulia kama analia au anatoa machozi muache alie hadi atosheke mwenyewe hiyo ndio dawa muhimu kwake ya kumfanya atoe kilicho moyoni.

Muhimu
Inashauriwa mara baada ya kutoa machozi hakikisha unakuwa na mood nzuri,

mchangamfu kwani machozi pia husaidia 'ku-clear mind' (kusafisha akili).


No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.