FAHAMU JINSI YA KUISHI NA HIV (UKIMWI)






Tarehe 1 desemba kila mwaka, ni siku ya ukimwi duniani.Ukimwi na magonjwa mengine makubwa yamepewa siku rasmi kila mwaka ili kuikumbusha jamii juu ya mapambano dhidi ya magonjwa hayo. Katika siku hizo pia hutolewa matokeo ya tafiti mbalimbali zinazohusu magonjwa husika.


Juzi tumeambiwa kuwa kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kimeshuka kutoka 5.7% hadi 5.1%. Ndio kusema katika kundi la watanzania ishirini, mmoja ameambukuzwa virusi vya ukimwi. Swali, je! Mtanzania huyo mmoja kati ya ishirini ameelimishwa vya kutosha juu ya njia za kuishi na maambukizi hayo?

Namna ya kuishi na maabukizi ya ukimwi.
Virusi vya ukimwi vina nguvu za kipekee sana, pamoja na mwili kuwa na kinga yake ya asili ya kupambana na virusi hivyo lakini mara nyingi kinga hiyo hushindwa na kumfanya mwathirika apate anguko la kiafya. Kuna mbinu kadhaa ambazo mwathirika  anaweza kuzitumia ili kuongezea kinga yake nguvu ya kupambana na virusi.



Mwathirika afanye nini anapogundua hali yake ?
Mara tu baada ya kugundua kuwa umeambukuzwa virusi vya ukimwi ni vema kutafuta mtaalamu wa afya akuelekeze mambo kadhaa pamoja na ushauri na nasaha. Pia mtaalamu hujenga saikolojia ya mwathirika na kumuondolea uwezekano wa msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo ni hatari kwa kuwa hupelekea mwili kuzalisha homoni aina ya steroids ambazo hupunguza kinga ya asili ya mwili, na hivyo kuvipa virusi nafasi kubwa ya ushindi.



Mwathirika ajijengee tabia gani?
Ni vema mwathirika wa virusi vya ukimwi ajenge tabia ambazo zitamletea furaha muda mwingi. Kwa mfano michezo, kusoma hadithi za kuvutia, kushiriki matamasha ya burudani, kusikiliza muziki mzuri na hata kufanya kazi ndogondogo za mikono. Mambo haya hujenga afya kubwa ya kisaikolojia ambayo hupelekea kinga ya mwili kuimarika.

Vyakula na vitu vingine visivyofaa kwa mwathirika wa VVU?
Vyakula hujenga mwili na ladha yake huleta furaha, Hata hivyo ni vema kwa baadhi ya waathirika kupunguza au kuacha kutumia baadhi ya vyakula. Mfano NYAMA NYEKUDU, itokanayo na Mbuzi, Ngombe, kondoo nk. Nyama hizi zina kiasi kikubwa cha lehemu(cholesterol) ambayo huganda ndani ya mirija ya damu na kupunguza ufanisi wa mzunguko wa damu. Pia Nyama hizi ni ngumu kiasi cha kuhitaji nguvu nyingi ili ziweze kumeng’enywa mwilini.



KAHAWA NA CHAI, zina kemikali aina ya nicotine na caffeine ambazo huzuia baadhi ya virutubishona vitamini kufanaya kazi mwilini.



Vyakula vya viwandani vyenye sukari na kemikali nyingi, huweza kusababisha kitambi (obesity) na Mgandamizo mkubwa wa damu (Hypertension). Matatizo haya huweza kupelekea mwili kupoteza uwezo wa kupamabana vema na VVU kwani huathiri mzunguko wa damu na kupunguza ufanisi wa kusambaza virutubisho mwilini. Pia baadhi ya ogani kama figo, ini na moyo vinaweza kuzidiwa uwezo na kusabaisha madhara zaidi.



SIGARA si jambo la kupunguza, bali kuacha kabisa kwani huharakisha uwezekano wa kupata TB. Mwathirika wa VVU akipata na TB anakuwa katika hatari ya kupoteza maisha kwa haraka. Kwa bahati mbaya katika Tanzania, asilimia kubwa sana ya waathirika wa VVU waanaugua piaTB. Sigara pia huweza kusababisha kansa na magonywa mengine mengi ya mapafu na nje ya mapafu.

POMBE ni vema kupunguza au kuacha kabisa. 
Pombe kupita kiasi pamoja na sigara huzuia baadhi ya virutubisho kufanya kazi mwilini. Pia pombe hupunguza ufanisi wa ini kuweza kusafisha damu na zaidi hupunguza hamu ya kula. Mambo hayo ni hatari kwa mwathirika wa VVU ambaye anahitaji chakula bora ch kutosha  na mwili imara.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.