Epuka malezi ya aina hii kwa Mwanao


Kuna baadhi ya wazazi huwalea watoto wao katika misingi ambayo imekiwa haijengi hata chembe, hivyo ili kujenga kizazi chenye tija ogopa sana kulea mtoto katika msingi hii, kwani kila kitu katika maisha ya mtu huanza kwa mtoto akiwa mdogo, hivyo jitahidi kumlea mwanao vizuri tangu akiwa mdogo.

1.Tabia ya Kumpongeza Mtoto na Kumuadhibu:
Pongezi ni muhimu katika kujenga tabia nzuri ya mtoto na hata akiwa mtu mzima kama ambavyo ni muhimu katika kuadhibu. Mtoto anajifunza kuwa akifanya kitu vizuri au akifanya vitu vizuri anapata zawadi na kinyume chake anaadhibiwa. Hii ni kweli hata katika utu uzima.

Japo pongezi isizidi mipaka na kumuharibu mtoto ( soma jinsi pongezi zinvyoharibu watoto ) ni vyema mtoto akajua kuwa kunamatokeo chanya na hasi kwenye kila anachokifanya na pale anaposhindwa kufikia malengo basi aongeze bidii zaidi na atafanikiwa.

Pongezi inaweza ikawa ni makofi tu au maneno ya kumtia moyo kama “Hakika wewe ni mtoto mzuri, ninajivunia”. Pongezi zinamfanya mtoto kupenda kufanya vitu vizuri tena siku nyingine. Adhabu ni muhimu pia,hasa pale ambapo mtoto ameelezwa mara kadhaa na haoneshi mabadiliko yoyote.  Adhabu ni kitu hasi chenye nia ya kukuongoza katika njia chanya.

Maisha ya binadamu yanaongozwa na sheria,sheria ziko kila mahali,nyumbani,kazini,barabarani na sehemu nyingine nyingi kwa madhumuni ya kuleta utaratibu fulani wa kuishi. Adhabu inamjenga mtoto kufahamu kuwa kunasheia na ni budi kuzifuata vinginevyo utaingia matatani.

2. Tabia ya Uchoyo,Ulafi na Ubinfsi:
Unajua mafisadi na majambazi wanatengenezwa wapi? Ni katika familia zetu. Tunamuona mtoto hataki kula na wenzake na ananyang’anya wenzake kile walichonacho hata kama hana kazi navyo na tunakaa kimya. Unategemea nini mtoto huyu akiwa waziri au raisi wa nchi?

Wazazi wanatakiwa kukemea tabia za uchoyo na ulafi kwa watoto. Mfundishe mtoto kucheza,kula na kupeana vitu na wenzake. Mjengee moyo wa kutoa na kuwa na kiasi kwani hivi vina mchango mkubwa katika kumjenga kuwa mtu mzima mwenye haiba.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.