BAO LA ASANTE KWASI LAWEKA REKODI NNE KALI




Watu na bahati zao bwana, goli alilofunga beki wa Simba Asante Kwasi dhidi ya Jamhuri limeingia kwenye rekodi kadhaa. Beki huyo ambaye usajili wake kutoka Lipuli kwenda Simba ulipamba headlines za michezo Bongo amefunga goli lake la kwanza akiitumikia Simba kwa mara ya kwanza ikiwa ni mechi yake ya kwanza ya Mapinduzi Cup lakini akicheza kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.
Mtangazaji wa Azam TV Pascal Kabombe wakati akitangaza goli hilo alisikika akisema: “Asante Kwasi amefunga goli lake la kwanza akiichezea Simba kwa mara ya kwanza lakini ni mara yake ya kwanza kucheza kwenye uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.”
Goli hilo lilikuwa ni la tatu kwa Simba katika mchezo huo baada ya John Bocco na Moses Kitandu kutangulia kufunga magoli mawili ya mapema.
Simba imefikisha pointi nne baada ya kucheza mechi mbili, mchezo wa kwanza walilazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 na Mwenge. Pointi nne zinawafanya wapane hadi nafasi ya pili nyuma ya Azam ambao wana pointi sita wakiwa wamecheza mechi mbili pili mbili.
Kwasi ndio mambo yake kufunga, akiwa na Lipuli tayari alishafunga magoli matano kwenye ligi kuu ya Tanzania bara akiwa ndiye beki mwenye magoli mengi zaidi hadi sasa. Magoli hayo (matano) yanamfanya kuwa nyuma kwa magoli matatu dhidi ya mchezaji anaeongoza kwa magoli hadi sasa ambaye ni Emanuel Okwi wa Simba.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.