Tshishimbi, Ajib, wanakimbiza soko la jezi, Okwi kaporomoka
Wachezaji wapya wa Yanga Ibrahim Ajib na Papy Kabamba Tshishimbi wanakimbiza kwenye soko la jezi mkoani Singida kuelekea mechi ya ligi kuu Tanzania bara kati ya Singida United vs Yanga mechi itakayochezwa Jumamosi ya October 4, 2017.
Ukizunguka nje ya uwanja wa Namfua unakutana na wauza jezi kibao ambao wamezimwaga chini jezi za Simba na Yanga, www.shaffihDauda.co.tz imefanya utafiti kwa baadhi ya wauzaji na kugundua jezi zinazonunuliwa sanana mashabiki wa Singida ni za Ajib na Tshishimbi.
“Jezi zinazouzika sana ni za Papy Tshishimbi na Ibrahim Ajib, hadi sasa hivi (jioni November 3, 2017) nimeuza jezi 15 za Tshishimbi na 10 za Ajib,” Ally Ngasa mmoja kati wauza jezi aliyezungumza na mtandao huu.
Mfungaji anaeongoza kwa magoli VPL Emanuel Okwi anaekipiga Simba mauzo ya jezi yake yameshuka kwa mujibu wa wauza jezi za Simba na Yanga waliokuwepo nje ya uwanja wa Namfua,wauzaji watatu kati yao wamesema Okwi anaongoza kwa upande wa Simba lakini kiujumla ameshuka ukilinganisha na alivyokuja mwanzoni.
“Kwa upande wa Simba jezi inayotoka sana ni ya Shiza Kichuya na Haruna Niyonzima, Okwi soko lake limepungua kidogo tofauti na alivyokuja” amesema Bw. Ally Ngasa kaka wa mchezaji Mrisho Ngasa wa Mbeya City.
“Jezi za Simba na Yanga zinapatikana kwa urahisi tofauti na za timu nyingine kama Singida United.”
No comments