Rekodi 8 ambazo Messi bado hajavunja: CR7 kizingiti kwenye rekodi 3


Lionel Messi ametimiza mechi 600 akiwa na FC Barcelona Jumamosi iliyopita wakati Barca walipoifunga Barcelona 2-1 katika La Liga. Tayari ameshavunja na kuweka rekodi kadhaa, lakini bado hizi hapa rekodi 8 hajafanikiwa kuzivunja au kuziweka…..
All time Top goalscorer katika Champions League:



 Mpaka sasa Cristiano Ronaldo mwenye magoli 110 anaongoza, Messi akifuatia na magoli 97. Hata hivyo CR7 amemzidi Messi mika miwili na huenda La Purga akafanikiwa kuivunja rekodi hii misimu kadhaa ijayo wakati CR7 akiwa tayari muda umemtupa mkono.
Mchezaji mwenye makombe mengi katika historia ya soka:


Messi tayari ameshashinda makombe 30, idadi sawa na Gerard Pique. Ryan Giggs ameshinda makombe 36 na United, Victor Baia alishinda vikombe 35, Andres Iniesta makombe 32, Gary Neville akiwa na United, Dani Alves (PSG, ex Barca), wote walishinda makombe 31.
Mchezaji mwenye vikombe vingi vya ulaya (UCL/EuropeanCups):



Paco Gento wa Madrid alishinda vikombe 6, Di Stefano, Jose Maria Zarraga (wote Real Madrid) na Paolo Maldini (AC Milan) wote wana rekodi ya kushinda makombe 5, wakati Messi, Ronaldo, Iniesta na Pique wote wakiwa wameshinda mara 4.
Mchezaji mwenye vikombe vingi vya ulaya (UCL/SuperCups): 


Dani Alves, Paulo Maldini na Arie Haan (Ajax) wote wameshinda kwa ujumla makombe 9 kila mmoja. Kwa sasa Messi tayari ameshinda 7, manne ya Champions League na matatu ya Super Cups, idadi sawa na Pique, Iniesta na Cristiano.
Mfungaji bora wa klabu moja: 



Messi tayari amefunga magoli 523 katika mechi 600, Gerd Muller alifunga magoli 525 katika mechi 563 alizoitumikia Bayern. Anayeshikilia rekodi mpaka sasa Josef Bican, ambaye kati ya mwaka 1937 na 1948 alifunga magoli 534 katika mechi 274 na klabu ya Slavia Prague. Pele alifunga magoli 643 katika mechi 659 akiwa na Santos kutoka 1956 mpaka 1974.
Mchezaji aliyeitumikia Barcelona mechi nyingi:




Xavi Hernandez ndio anashikilia rekodi hii akiwa amecheza mechi 767. Anayemfuatia ni Iniesta 642 halafu Messi, 600.
Mchezaji aliyeshinda mechi nyingi nchini Spain: 



Iker Casillas ana rekodi ya kushinda mechi 334 akiwa na Real Madrid kabla ya kwenda Porto. Andoni Zubizarreta (Athletic, Barcelona, Valencia) alimaliza kucheza soka na ushindi katika mechi 333. Raul Gonzalez 327, Xavi 322 na Manolo Sanchis 312 wa Madrid nae yupo mbele ya Messi, ambaye mpaka sasa ameshashinda mechi 298 za La Liga.
Mchezaji mwenye viatu vingi vya dhahabu:


Leo Messi alishinda tuzo hii (2009/10, 2011/12, 2012/13 na 2016/17) na Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo hii (2007/08, 2010/11, 2013/14 and 2014/15)  – sasa wote wanaipigania rekodi hii. Msimu huu tayari Messi amefunga magoli 12 kwenye La Liga, CR7 amefunga moja tu.
Mchezaji mwenye Ballon D’or nyingi: 


Hii ni vita nyingine ya Ronaldo vs Messi. La Purga alishinda tuzo hii mara 5 tayari 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015, wakati Cristiano alishinda 2008, 2013, 2014 na 2016, na mwaka huu pia anapewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda pamoja na kuanza msimu vibaya.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.