(PICHA + VIDEO):: SAMATTA TAYARI KAFANYIWA UPASUAJI WA GOTI, KWA MAFANIKIO



Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta siku ya Jumamosi ya November 4 2017 katika uwanja wao wa Luminus Arena alikuwa uwanjani kuitumikia Genk lakini kwa bahati mbaya hakumaliza game.
Samatta aliichezea KRC Genk katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya Lokeren mchezo ambao ulimalizika kwa sare tasa (0-0) lakini nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye alikuwa akiongoza safu ya ushambuliaji ya Genk alishindwa kumaliza dakika 90 na kuishia kucheza kwa dakika 40.
Uchunguzi ulifanywa na jopo la madaktari wa Genk na kueleza kuwa Samatta atahitaji upasuaji wa goti lake la kulia baada ya kuumia goti hilo na atakuwa nje ya uwanja hadi mwanzoni mwa kipindi cha majira ya baridi, good news ni kuwa Samatta leo amethibitisha kuwa upasuaji wake umeenda salama.
“Napenda kuwajulisha kuwa operesheni yangu imeenda vizuri. Napenda kumshkuru mwenyezi Mungu, timu ya madaktari pamoja na mashabiki wangu, nimepokea meseji nyingi sana kutoka sehemu tofauti duniani na napenda kuchukua fursa hii kuwashkuru sana kwa meseji na Dua zenu”>>> Samatta




No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.