MATOKEO YA JANA EPL NA MSIMAMO WAKE BAADA YA ROUND YA 13, ARSENAL YARUDI TOP 4, CITY WAZIDI KUJICHIMBIA KILELENI



Manchester City nao waliibuka kidedea kwa bao 2 kwa  zidi ya Huddersfield ambao leo wamekuwa timu ya kwanza kuifunga City bao la set piece huku Aguero akiwa mchezaji wa kwanza kufunga penati 3 mfululizo tangu Yohane Cabaye afanye hivyo 2015.

Bao la dakika ya 90 la Alexis Sanchez liliwahakikishia Arsenal kuibuka kidedea katika mchezo wao wa leo zidi ya Watford ushindi ambao umewarudisha hadi nafasi ya nne wakiwa na alama(25).



Everton waliokuwa ugenini waliendela kuboronga baada ya hii leo kuchapwa mabao 4 kwa 1 na Southampton, huku mabao ya Southampton yakifungwa na Charlie Austin(2), Steven Davis na Dusan Tadic.


Kwa matokeo ya hii leo Manchester City wanazidi kung’ang’ania kileleni mwa msimamo wa Epl wakiwa na alama 37 wakifuatiwa na Manchester United katika nafasi ya pili na alama 29.


MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND BAADA YA ROUND YA 13


No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.