MAJINA YA WANASOKA 5 WANAOWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA(BBC) YAWEKWA HADHARANI

Jopo la wataalamu wa soka wakiongozwa na mkongwe wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Emmanuel Emunike wamekaa chini na kujadili majina ya wachezaji watano wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika msimu huu.



1.Naby Keita. Amekuwa gumzo kubwa katika ligi ya Ujerumani Bundesliga kutokana na kiwango alichokionesha akiwa na Rb Leizpg na msimu huu alikuwepo katika kikosi cha Bundesliga. Keita pia anahusishwa na kujiunga na Liverpool.



2.Sadio Mane. Alikuwepo katika kikosi cha Epl cha waandishi wa habari za michezo, alichaguliwa mchezaji bora wa klabu ya Liverpool msimu uliopita huku pia hapo jana akiisaidia Senegal kufuzu kwa fainali za kombe la dunia




3.Pierre Aubameyang. Msimu uliopita alifanya makubwa Ujerumani akifunga mabao 35 na kuweka rekodi kuwa mchezaji wa 4 kuwahi kufunga mabao 30 nchini Ujerumani huku akiwa Muafrika wa kwanza kufikisha mabao hayo katika Bundesliga



4.Mo Salah. Ameiwezesha Misri kushiriki michuano ya kombe la dunia lakini msimu uliopita alikuwa na kiwango kizuri sana alipokuwa Fiorentina huku msimu huu akiwa amefunga mabao 7 katika ligi ya Epl.


5.Victor Moses. Kama ilivyo kwa Salah na Mane huyu naye tayari timu yake imefuzu kuelekea Urusi, Victor Moses tangu kocha Antonio Conte ajiunge na Chelsea amekuwa akimpa sana nafasi japokuwa msimu huu ameandamwa na majeraha yanayomuweka nje hadi sasa.


No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.