KAMA BADO HUJAONA GOLI LA BOCCO LILILO VUNJA RECORD YA TOKEA 2013 HILI HAPA




TAZAMA HAPA



John Bocco ameipa Simba ushindi wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons tangu iliposhinda mara ya mwisho 2013 kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.
Bao pekee la ushindi limefungwa dakika ya 84 kipindi cha pili baada ya Bocco kuuwahi mpira uliochelewa kuokolewa na mabeki wa Prisons.
Simba imepata pointi sita kwenye uwanja wa Sokoine baada ya kusubiri kwa muda mrefu. Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe pointi 22 ikiwa inaongoza ligi mbele ya Azam ambayo itacheza kesho dhidi ya Njombe Mji.
Yanga inabaki katika nafasi ya tatu huku Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya nne timu zote zikiwa na pointi 17 lakini zinatofautiana kwa wastani wa magoli. (Azam, Yanga na Mtibwa Sugar ni timu tatu ambazo zipo top four zikiifukuza Simba kileleni kwenye msimamo wa VPL).
  • Simba imepata ushindi wa sita katika mechi 10 walizocheza, sare nne huku ikiwa haijapoteza mchezo.
  • Ushindi dhidi ya Prisons ni wa tatu nje ya uwanja wa Uhuru (Stand United 0-1 Simba, Mbeya City 0-1 Simba, Tanzania Prisons 0-1 Simba).
  • Hawajashinda mechi mbili walizocheza nje ya uwanja wa Uhuru (Azam 0-0 Simba, Mbao 2-2 Simba).
  • Bocco amefunga goli lake la pili VPL tangu alipojiunga na Simba, alifunga bao lake la kwanza September 17, 2017 Simba ilipocheza dhidi ya Mwadui na kushinda 3-0 uwanja wa Uhuru.
Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa leo Jumamosi Nov 18, 2017.
  • Stand United 0-0 Mwadui
  • Ruvu Shooting 1-0 Ndanda
  • Majimaji 2-1 Mbao

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.