VIDEO:: KAMA HUKUONA MAGOLI YA SIMBA VS YANGA, HAYA HAPA ,


Mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara mzunguko wa nane baina ya mwenyeji Yanga SC dhidi ya Simba SC umemalizika Uwanja wa Uhuru kwa kutoshana nguvu ya sare ya bao 1-1.
Katika mchezo huo wa watani wa jadi umeamuliwa na wachezaji Shiza Ramadhani Kichuya aliyeanza kuona lango la Yanga katika dakika ya 57 ya kipindi chapili baada ya kupachika bao safi kisha dakika chache tu,Obrey Chirwa akawainua mashabiki wa Yanga kwa kuipatia bao katika dakika ya 60 na kufanya matokeo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Baad ya ushindi huo makocha wapande zote mbili walipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari.
Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga Shadrack Nsajigwa amesema “Mchezo ulikuwa mgumu kwa kuwa timu zote zilijiandaa kwaajili ya kupata matokeo ya ushindi.”Amesema Nsajigwa.
Nsajigwa ameongeza “Nawapongeza sana wapinzani wangu kwakuwa ni timu nzuri ila nivigumu sana kubashiri nani angekuwa nyota wa mchezo naamini anaweza kutoka upande wowote.”
Kwa upande wa Kocha wa Simba SC, Joseph Omog amesema ” Ulikuwa mchezo mzuri,mgumu na ushindani tulipata nafasi nyingi lakini hatukuzitumia.”
Hata hivyo Omog alipoulizwa na waandishi juu ya safu yake ya ulinzi kupwaya na hata upande wa ushambuliaji kushindwa kufunga mabao kama ilivyozoeleka amesema ni kutokana na mchezo wenye.
Kufuatia matokeo ya leo klabu ya Simba inarejea kileleni mwa msimamo wa ligi kwakuwa na alama 16 sawa na Yanga Sc na Azam FC ila ikiwa na tofauti nzuri ya mabao


No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.