SIMBA YAPAA BAADA YA USHINDI WAO DHIDI YA STAND UTD SHINYANGA



Stand United wameiruhusu Simba iongoze ligi kuu Tanzania bara baada ya kuchapwa 2-1 kwenye uwanja wao wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.
Pointi tatu walizozipata Simba zimewafanya kufikisha jumla ya pointi 11 sawa na Mtibwa Sugar pamoja na Azam. Simba wanapanda kutoka nafasi ya sita hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kutokana na wastani wa magoli.
Shiza Ramadhani Kichuya amefunga goli la kwanza dakika ya 17 kipindi cha kwanza. Dakika ya 42 Laudit Mavugo aliifungia Simba bao la pili dakika mbili baada ya kuingi kutoka benchi kuchukua nafasi ya Emanuel Okwi.
Stand United walipata bao pekee dakika ya 52 kipindi cha pili kupitia kwa Mutasa Munashe. Stand walipata mkwaju wa penati baada ya beki wa Simba kushika mpira kwenye eneo la hatari. Munashe akapiga penati ambayo ilipanguliwa na Manula lakini akamalizia tena kuifungia Stand.
  • Simba imeshinda dhidi ya Stand katika mechi tano za hivi karibuni za ligi kuu Tanzania bara.
  • Mara ya mwisho Stand kupata ushindi dhidi ya Simba ilikua 21/02/2015 ambapo Stand walishida 1-0 kwenye uwanja wa Kambarage.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.