HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIO PATA MKOPO AWAMU YA KWANZA KUTOKA HESLB



Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema baada ya uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018, orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo imekamilika.



Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Jumatano Oktoba 18,2017 amesema Sh34.6 bilioni zimetengwa kwa ajili ya wanafunzi hao 10,196.

Amesema kwa jumla Sh108.8 bilioni zitatolewa kwa wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Amesema orodha nyingine (batches) zitafuata kwa kadri utaratibu wa udahili na uchambuzi unavyokamilika.


Badru amesema orodha ya awamu ya kwanza inapatikana kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo http://www.heslb.go.tz/ na itatumwa kwa vyuo husika.

BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA PDF FORMAT




No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.