Matokeo ya leo yamfanya Kane kumkaribia Messi huku Lukaku akivunja rekodi ya Andy Cole

Tottenham wameweka rekodi mpya katika Epl kwa kushinda michezo 6 mfululizo ya ugenini baada ya hii leo kuibuka tena kidedea kwa ushindi wa mabao manne kwa sifuri dhidi ya Huddersfield.
Katika mchezo ambao ulionekana wazi ni wa upande mmoja, Harry Kane alifunga mabao mawili na kumfanya kuwa mshambuliaji wa pili Ulaya kuwa na mabao mengi(36) mwaka huu baada ya Lioneil Messi mwenye 46.

Mabao mengine ya Tot yaliwekwa kimiani na Ben Davies huku Moussa Sissoko akifunga bao lake la kwanza katika michezo 44 tangu ajiunge na Tottenhma Hotspur.
Baada ya mechi kati ya Huddersfield na Tottenham Hotspur kulifuatia mchezo kati ya Manchester United waliokuwa nyumbani Old Traford dhidi ya Crystal Palace.
Haikuchukua muda kuanza kumuona mshindi kwani sekunde 180 tu zilimtosha Juan Mata kufunga bao la kwanza kwa United ikiwa pia ni bao lake la kwanza katika msimu huu wa Epl.

Marouane Fellaini aliongeza mawili kabla Lukaku kufunga la nne na kuifanya timu hiyo kushinda magoli manne kwa mara ya 3 msimu huu huku msimu uliopita walishinda magoli manne Old Trafford mara moja tu.
Goli alilofunga hii leo Romelu Lukaku lilikuwa bao lake la 7 katika michezo yake 7 ya mwanzo ya Epl na kumfanya kufikia rekodi hiyo ambayo hapo kabla ilikuwa ikishikiliwa na Andy Cole.

Swansea waliendelea kupigika baada ya leo kuchezea kichapo cha bao 1 kwa sifuri toka kwa West Ham huku West Bromich na Watford wakienda sare ya bao mbili kwa mbili, Stoke City nao wakiwa nyumbani waliichapa Southampton bao 2 kwa 1.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.