MADRID YAPIGWA NA BETIS, YAVUNJIWA RECORD... PAMOJA NA MATOKEO MENGINE YOTE BARANI ULAYA
Usiku wa September 20 2017 club ya Real Madrid ilirudi katika uwanja wake wa Santiago Bernabeu kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya Real Betis, Madrid walirudi wakiwa na staa wao Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa amefungiwa game nne na LaLiga.

Real Betis wamefanikiwa kuondoka na point tatu Santiago Bernabeu baada ya kuifunga Real Madrid kwa goli 1-0, goli la Real Betis likifungwa dakika ya 90 na Sanabria Ayala, kipigo hicho kinavunja rekodi mbili za Real Madrid ambapo game hiyo ndio inakuwa ya kwanza kumalizika kwa Real Madrid kutofunga goli toka April 2016 dhidi ya ManCity (0-0).



No comments