MANENO YA MWISHO KUTOKA KWA MESSI KWENDA KWA RAFIKI AKE KIPENZI NEYMAR BAADA YA BARCELONA KUMWACHIA NEYMAR KWA PSG



Kwa sasa taarifa kuu katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii Ulaya ni kuhusiana na ishu ya mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona Neymar kuhusishwa kukaribia kujiunga na Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Habari kutoka katika mitandao mingi ya Ulaya inaripoti kuwa PSG hadi sasa wana asilimia 90 ya kumpata Neymar kutokana na mchezaji huyo kuiomba na kuishinikiza Barcelona imuuze, baada ya kocha kumpa ruhusa Neymar na FC Barcelona kuthibitisha Neymar kuombwa kuuzwa.



Lionel Messi ambaye amecheza na Neymarkwa miaka minne toka staa huyo ajiunge na Barcelona, ametumia ukurasa wake wa instagram kumtakia kila la kheri Neymarambaye leo inaaminika ameshasafiri kuelekea Paris kukamilisha uhamisho huo.

“Ilikuwa ni heshima kushea chumba kimoja cha kubadilishia nguo na wewe kwa miaka yote hiyo rafiki yangu Neymar kila la kheri katika hatua mpya ya maisha yako”>>>Messi



No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.