HIZI HAPA SHULE KUMI (10) BORA ZA KWANZA NA KUMI(10) ZA MWISHO MATOKEO YA FORM SIX 2017

Matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2017 yametoka leo Jumamosi, Julai 15 huku shule ya Wasichana ya Feza Girls ikiibuka kinara kwa watahiniwa wake 67 kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili.


Shule nyingine zilizoibuka kidedea katika matokeo hayo ni Marian Boys, iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri (Arusha) imeshika nafasi ya tatu na Ahmes (Pwani) imeshika nafasi ya nne.

 Shule nyingine  ni  Marian  Girls (Pwani) iliyoshika nafasi ya tano, Mzumbe (Morogoro) nafasi ya sita, St Marry Mazinde Juu (Tanga) nafasi ya saba, Tabora Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza BOYS (Dar es Salaam) nafasi ya tisa na Kibaha ya Pwani iliyoshika namba kumi.







Shule 10 za Mwisho matokeo ya kidato cha sita


Ni kilio na kicheko. Hivyo ndivyo tutakavyoweza kusema, kwani matokeo ya kidato cha sita, yaliyotangazwa leo Jumamosi, Julai 15 yamezitaja shule kumi zilizofanya vibaya na kushika mkia kitaifa.

Shule hizo ni Kiembesamaki Unguja, Hagafilo (Njombe), Chasasa (Pemba), Mwenyeheri Anuarite (Dar es Salaam) na Ben Bella (Unguja).

Nyingine zilizotajwa kushika mkia ni Meta (Mbeya), Mlima Mbeya(Mbeya)

 Nyingine ni Shule ya Sekondari ya Al-Ihsan Girls (Unguja na St Vicent(Tabora).

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.