PICHA NA VIDEO Tanzania 4 vs 2 Lesotho: COSAFA 2017 - Taifa Stars Yanyakua Nafasi Ya Tatu



Tanzania imeshinda kwa mikwaju ya penati 4-2 dhidi ya Lesotho baada ya kutoka sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kwenye michuano ya COSAFA Cup 2017 kwenye uwanja wa Moruleng.
Matokeo hayo yanaifanya Stars kumaliza nafasi ya tatu kwenye mashindano huku Lesotho wakimaliza katika nafasi ya nne.

Golikipa wa Stars Said Mohamed alikuwa kikwazo kwa Lesotho kutokana na kuokoa michomo kadhaa wakati ‘Mamba’ wakitafuta goli la kuongoza.
Lesotho waliendelea kuliandama lango la Stars na dakika ya 24 Jane Thaba-Ntso alimlazimisha Mohamed Said kufanya kazi ya ziada kuokoa mchomo.

Presha kwa Taifa Stars iliendelea kuwa kubwa ambapo dakika ya 35 alimnyima goli Thaba-Ntso kwa mara ya pili.
Stars walianza kipindi cha pili shambulizi, Salmin Hoza alipiga kiki ambayo iliokolewa na golikipa kwa Lesotho Sam Ketsekile.

Wakati kikosi chake kikipambana kupata bao, kocha mkuu wa Lesotho Moses Maliehe alimjingiza Mabuti Potloane.
Kwenye hatua ya mikwaju ya penati, Mohamed Said alipangua penati moja ya Thapelo Mokhehle na Raphael Daud akafunga penati ya mwisho kuipa ushindi wa penati 4-2.


No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.