(VIDEO) ANGALIA MAGOLI YA SAMATTA NA ROONEY,,,KRC GENK VS EVERTON


Leo Julai 22, 2017 Mbwana Samatta ameandika rekodi ya kufunga goli dhidi ya klabu inayoshiriki ligi kuu ya England baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Everton katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa kwenye uwanja wa Luminus Arena ikiwa ni maandalizi kwa timu zote kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Samatta alifunga goli la kuisawazishia Genk dakika ya 55 baada ya Wayne Rooney kuifungia bao Everton dakika ya 45 kipindi cha kwanza. Everton ambayo inadhaminiwa na kampuni ya SportPesa, imeendelea kucheza mechi za kirafiki kujiandaa na msimu ujao wa EPL muda mfupi baada ya kucheza na Gor Mahia kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.