KWA HUYU,..YANGA YAPATA KIPA


Baada ya kuachana na makipa wake Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’ , Klabu ya Yanga imefanikiwa kumalizana na  kipa wa Serengeti Boys, Ramadhani  Kabwili baada ya kumsainisha kandarasi la kuichezea .
Uwezo wa Kabwili ulionekana kwenye michuano ya Afrika kwa vijana wenye chini ya miaka 17 iliyofanyika mwaka huu nchini Gabon baada ya kuidakia Seregeti boys mechi zote .Kwa uwezo aliouonyesha , Tayari Kabwili ameitwa kwa mara ya kwanza  kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoweka kambi jijini Mwanza kujiandaa na mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Rwanda ‘Amavubi’ utakaopigwa Jumamosi .
Ukiachana na usajili  wa Kabwili , Tayari yanga wana makipa wawili ambao ni Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon na Benno Kakolanya ambaye anaendelea kuitumikia klabu hiyo .

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.