KOCHA WA SIMBA "OMOG" AWATUMIA SALAMU ZA "VITISHO" WATANI WAO WA JADI YANGA




Kocha Mkuu  wa Klabu ya Simba,  Joseph Omog ambaye yupo nchini Afrika Kusini na kikosi chake wakijinoa kwa maandalizi ya mechi ya ngao ya hisani inayotarajiwa kuchezwa Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, amesema maandilizi hayo ni kwa ajili ya mchezo who dhidi ya Yanga pamoja na msimu mpya.


Kocha wa Simba, Joseph Omog wa kwanza toka kushoto akiwa kambini Afrika Kusini


Omog amesema kambi hiyo itawapa nafasi ya kujiandaa vizuri kwa kuwa wapo katika mazingira tulivu hivyo anaamini watawapa raha Wanamsimbazi kwenye mchezo wao wa ngao ya hisani.
Kambi hii inafaida kubwa (mbili), kwanza tunaandaa timu ambayo itawapa furaha mashabiki, hatujiandai kwa sababu ya mchezo wa Yanga peke yake, lakini ni maandalizi ya mchezo huo na pili kwa ajili ya Ligi Kuu,” amesema Omog kwenye mahojiano na Gazeti la Nipashe.
Hata hivyo, Omog amesema kambi hiyo itajenga msingi mzuri katika maandalizi yao ya kushiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika hapo mwakani.
Kwa upande mwingine, Klabu ya Yanga inaendelea kujifua jijini Dar es Salaam chini ya Mzambia George Lwandamina, na tayari kocha huyo ameeleza wamemaliza mazoezi ya kujenga mwili gym na sasa wanahamia program za uwanjani.

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.