STARS YATINGA ROBO FAINALI (COSAFA)









Tanzania, Taifa Stars imefanikiwa kuingia hatua ya Robo fainali ya kombe la Halmashauri ya Shirikisho la Vyama vya Mpira wa miguu kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya Kulazimisha kwenda Sare ya 1-1 dhidi ya Mauritius kwa goli lililofungwa na Simon msuva dakika ya 68' dakika moja tu baada ya Mauritius kuandika goli la kuongoza (dk 67') kupitia kwa Kelvin Perticots, huku Angola nayo ikilazimishwa sare ya bila kufungana na Malawi. 


Kwa matokeo hayo Tanzania inaongoza kundi 'A' kwa tofauti ya goli moja dhidi ya Angola ambayo nayo ina alama sawa na Tanzania


FT: Tanzania 1 - 1 Mauritius
FT: Malawi 0 - 0 Angola

Tanzania itakutana na Afrika Kusini katika Mchezo wa Robo Fainali tarehe 5 July.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Taifa Stars.



No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.