ZIJUE FAIDA ZINGINE ZA MAJI KATIKA MWILI WA BINADAMU




Moja kati ya kauli mbiu ambayo ipo katika matumizi ya  maji wanasema ya kwamba, maji ni uhai. Huo ni ukweli usiopingika juu ya kauli hiyo ijapokua watu wengi huwa hawatumii maji hayo.

Hivyo kama wewe ni miongoni mwa watu hao Makala haya yatakufaa kwani utakwenda kujua ukweli kuhusu faida za maji mwilini.

Faida za maji mwilini ni kama ifuatavyo;
1.    Unywaji wa maji husaidia kuifanya ngozi yako kuwa nyororo na nadhifu.

2.    Maji husaidia kwa kiwango kikubwa katika mfumo wa kuchanganya chakula katika mwili wa mwanadamu. Lakini pia maji husaidia kupunguza uwezekano wa kuapata saratani ya colonikwa asilimia 45.

3.    Maji husaidia kupunguza calories mwilini, yaani badala ya kunywa vimininika vingine kama vile soda, juisi na bia ambavyo vina calories, hivyo unashauriwa utumie maji kwani yenyewe hayana calories. Lakini pia unashauriwa ya kwamba kila wakati uendelee kutumia maji kwani yenyewe hayana mafuta, sukari ambavyo husababisha athari mbaya katika mwili wa binadamu.

4.     Kwa wale ambao hushambuliwa na maumivu ya kichwa, tunaambiwa ya kwamba maji husaidia kutibu maamivu ya kichwa, kwani inasdikia ya kwamba upungufu wa maji mwilini husababisha kichwa kuuma, hivyo kila wakati ni vyema ukatumia maji ili ujitibu.

5.    Utumiaji wa maji kwa kiwango kikubwa kila wakati humsaidia mtu kuweza kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo, hivyo unashauriwa kwa siku tunywe zaidi walau bilau nane kwa siku.

Asante sana kwa kuendelea kutembelea SIMON MAYUNGA OFFICIAL, nasi tunakwambia “maji ni uhai, tumia maji kila wakati kwa afya bora” 

No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.