UNITED YATOLEWA NA VIBONDE WANAOANGUKIA MKONONI MWA MAN CITY, Chelsea vs Arsenal



Usiku mbaya kwa mashabiki wa Manchester United baada ya kushuhudia wakitupwa nje ya michuano ya Carbao Cup na timu ambayo haipo ligi kuu ya Carbao Cup baada ya kukubali kipigo cha mabao mawili.
Hii ni mara ya pili kwa Jose Mourinho kukubali kupokea kipigo kwa timu ambayo haipo ligi kuu tangu atue Uingereza,muuaji wa United alikuwa Korey Smith ambaye wakati mashabiki wa United wakiwaza mechi kuisha suluhu aliwafunga bao dakika ya 92.


Matokeo ya leo yanawafanya Bristol City kwenda moja kwa moja katika nusu fainali ya michuano hiyo ambapo sasa mchezo wa nusu fainali watakutana na Manchester City huku Chelsea akikutana na Arsenal.
Sasa Bristol wanakuwa timu ya pili kuzitoa timu nne za ligi kuu kwa msimu mmoja baada ya Swansea ya 1991/1992 kufanya hivyo huku wakiwa timu ya pili kumfunga Mourinho huku wakiwa hawapo ligi kuu tangu Bradford walipomfunga Mou alipokuwa Chelsea 2014/2015.


No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.