MFAHAMU NYOKA MKUBWA ZAIDI KULIKO WOTE KUWAHI KUISHI DUNIANI



#FAHAMU Titanoboa ndio aina ya nyoka mkubwa zaidi kuwahi kuishi kwenye historia hapa duniani. Alikuwa anapatikana kwenye msitu wa Amazon, kwa sasa kizazi chake hakipo tena kwani wanasayansi ya wanyama wamesema aliwahi kuishi miaka milioni 58 iliyopita. Nyoka huyo alikuwa ana uwezo wa kumeza hata mamba mkubwa, na inaaminika ndio asili ya kizazi cha nyoka aina ya Boa constrictor, Python na Green Anaconda. Mwaka 2009 wakati mainjinia wakifanya shughuli ya ujenzi nchini Colombia, waligundua masalia ambayo yalikuja kugundulika ni masalia ya nyoka aina ya Titanoboa.  Nyoka huyo na kizazi chake licha ya kuwa ndio nyoka mkubwa zaidi, hana sumu ya kuweza kumuua binadamu, kitu pekee ambacho ni silaha yake ni nguvu zake ambazo huzitumia kuvunjavunja adui yake na kummeza.



No comments

Theme images by hdoddema. Powered by Blogger.